Tuesday , 15th Dec , 2015

Staa wa muziki Black Rhyno, baada ya kufanya poa ndani na nje ya mipaka ya nchi na kolabo yake ya kimataifa 'We Get It On' na wasanii wa Kusini mwa Afrika, amesema kuwa ameamua kurejea katika soko la nyumbani kwa kufungia mwaka na kazi yake mpya.

Staa wa muziki nchini Black Rhyno

Black Rhyno ambaye amejipanga kuachia kazi hiyo kesho inayosimama kwa jina 'Time Ya Kumake Dooh', amesema kuwa hii ni kazi yake mpya yenye mchanganyiko ambao ameufanya ndani yake ni maalum kwa ajili ya wapenzi wa muziki wa hapa nyumbani, akiwa pia amewashirikisha wasanii wa hapa nyumbani kukamilisha muundo wa lengo lake.