Friday , 11th Dec , 2015

Halmashauri ya mji wa Njombe inakabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa fedha za maendeleo na kushindwa kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wakati huku mpaka mwezi huu wamepokea asilimia tano ya fedha zote za maendeleo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Njombe Eluminata Mwenda.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Njombe Eluminata Mwenda wakati akiwasilisha taarifa ya utekeleza wa miradi kwa kipindi ambacho halmashauri ilikabidhiwa kwa watendaji huku madiwani wakiwa katika uchaguzi.

Taarifa hiyo iliyosomwa mbele ya madiwani wapya baada ya kuapishwa kwao Mwenda amesema kuwa kwa kipindi ambacho halmashauri haikuwa na madiwani wamepokea asilimia tano ya bajeti nzima ya utekelezaji wa maendeleo.

Aidha mwenda amesema kuwa halmashauri ya mji wa Njombe imefanikiwa kuhakikisha kuwa imebadilisha baadhi ya sheria ndogondogo za halmashauri hiyo ili kuhakikisha zinaboreshwa na kufanya kazi bila kuwapo kwa vikwazo.