Thursday , 26th Nov , 2015

Mchezaji wa Man United Wayne Rooney na beki wa Chelsea John Terry ni wachezaji pekee kutoka England waliotajwa kuwemo kwenye orodha ya wachezaji 55 wa watakaounda kikosi cha wachezaji 11 bora duniani.

Mchezaji wa Man United Wayne Rooney na beki wa Chelsea John Terry ni wachezaji pekee kutoka England waliotajwa kuwemo kwenye orodha ya wachezaji 55 wa watakaounda kikosi cha wachezaji 11 bora duniani.

Orodha hiyo imetolewa na shirikisho la wachezaji wa kulipwa duniani lijulikanalo kwa jina la FifPro kutokana na kura takriban 25,000 zilizopigwa na wachezaji wa kulipwa duniani kote.

Real Madrid imetoa wachezaji 12 katika orodha hiyo wakati Bayern Munich ikitoa wachezaji 11.

Manchester City inawakilishwa na wachezaji wanne ambao ni Vincent Kompany, Yaya Toure, David Silva na Sergio Aguero, wakati Chelsea ikiwakilishwa na Branislav Ivanovic, Eden Hazard na Terry .

Katika wachezaji 55, wachezaji 23 wanatoka ligi ya Hispania, 12 ni kutoka ligi ya Ujerumani, 10 kutoka ligi kuu ya England, Ligi ya ufaransa imetoa wanne, na watatu kutoka ligi ya Italia, na mkongwe Andrea Pirlo anayekipiga nchini Marekani hakusahaulika.

Upigaji kura kuwapata wachezaji hao ulianza mwezi Septemba mwaka huu na wachezaji walioruhusiwa kupiga kura ni wale ambao wamecheza si chini ya mechi 15 kwa mwaka huu.

Kikosi cha mwisho kitatangazwa January 11 mwakani katika sherehe za tuzo ya Ballon D'Or baada ya mchujo.