Monday , 16th Nov , 2015

Wagombea katika ngazi mbalimbali za uongozi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Temeke TEFA wametakiwa kufanya kampeni za kistaarabu kwa manufaa ya wadau wa soka.

Mwenyekiti kamati ya uchaguzi ya TEFA Mashaka Mgaya amesema, kampeni za wagombea zinatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho ambapo kila mgombea anatakiwa kufanya kampeni kwa kuzingatia katiba na kanuni za soka ili kuweza kumaliza kampeni bila kuwa na matatizo yatakayochangia vurugu.

Mgaya amesema, wapiga kura wanatakiwa kuwapima wagombea kwa uwezo wao wa kujieleza kwa ufanisi wao wa kazi.

Mgaya amesema, yeyote atakayethubutu kuvunja amani katika kipindi cha kampeni na hata uchaguzi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za mpira ili kufanya uchaguzi kwa amani na kupata viongozi walio halali.