Saturday , 29th Mar , 2014

Msanii ambaye anafahamika kwa kukaza muziki wake ndani ya misingi na midundo ya Hip Hop, ametangaza rasmi leo kuwa kwa sasa mtazamo wake umebadilika sana katika muziki, na ameamua kufanya muziki ambao haujajifunga mahali pamoja.

Kimbunga

Kimbunga amesema kuwa amekuwa katika game ya hip hop kwa miaka mingi sasa na pia baada ya kujiingiza katika swala zima la utayarishaji muziki ameona kuwa asijizuie katika kile anachoweza kufanya.

Msanii huyu pia ametambulisha leo kazi yake ya tofauti kabisa inayokwenda kwa jina Usitukane ambayo amemshirikisha Chegge Chigunda, na hapa anaeleza juu ya mabadiliko makubwa aliyofanya.

Tags: