
Bushoke ameyasemahayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio, na kusema kwamba anaona ni fursa nzuri kwa wasanii, kwani kuna mambo ya kimaendeleo zaidi.
"Mi nafurahia maendeleo, naona muziki unapiga hatua kwamba watu wanazidi kuutambua, na watu wengi sana hata kwa raia na viongozi, wanajua wapiganie wapi watu wanataka sana haki za wanamuziki, wanajua wanamuziki wawe vipi na pia teknolojia inazidi kuchange, kwa hiyo watu wanajitahidi kupigana na hilo lakini mi naona mpaka hapamulipo muziki uko sawa", alisema Bushoke.
Pamoja na hayo Bushoke amesema anaogopa sana maoni ya baba yake mzazi ambaye pia ni msanii mkongwe hapa nchini, pale anapotoa wimbo mpya lakini kwa upande mwengine amekuwa na mchango mkubwa katika muziki wake kutokana na uzoefu alionao kwenye fani hiyo.
"Mzee ni msaada mkubwa kwangu, ananisaidia sana kwa sababu yeye ndo kaanza kuimba muziki kwenye familia yangu, na pia niko proud na muziki aliofanya muziki kwa sababu anafanya nielewe miziki ya aina nyingi sana, kwa hiyo ye ndo kila kitu yani, hata vile anavyocrotisize yeye na anasikiliza nyimbo zangu nyingi sana, ila katika watu ambao naogopa coment zake kama hajaupenda ni yeye", alisema Bushoke.
Pia Bushoke alimalizia kwa kusema idea ya wimbo wa mume bwege ilikuwa ni ya rafiki yake J Silk, lakini alitokea kuupenda wimbo huo na kufikia uamuzi wa kubadilishana naye kumpa ya kwake aimbe.
"60% ya ile nyimbo sikuianzisha mimi, aliianzisha jamaa mmoja anaitwa Juma Silk (J Silk) ile nyimbo yenyewe ilikuwa inahusu mtoto, yenyewe ilikuwa na verse moja inayosema mimi mweusi mtoto katoka mwarabu, ilipoishia pale mimi nikaipenda ile nyimbo kwa hiyo nikaendelea na ile nyimbo, na J silk kuna nyimbo yangu na mimi nikampa", alisema Bushoke kwenye Planet Bongo ya EA Radio.