Msanii wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya
Jaguar amefikia hatua hiyo baada ya kutembelea waathirika mjini Mombasa na kutathmini hali yao halisi, ambapo kutokana na uzito wa tatizo amelazimika kuwatafutia msaada waathirika hao kutoka taasisi ya pembeni ambacho kitahudumia waathirika wapatao 250 kwa kuanzia.
Star huyo anaendesha shughuli hiyo chini ya mamlaka inayosimamia kampeni dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya na Pombe nchini humo NACADA kama moja ya wajumbe wake, nafasi ambayo amepewa na Rais Uhuru Kenyatta.