Saturday , 18th Jul , 2015

Mwanamuziki wa muziki wa dansi Ramadhani Masanja maarufu kama 'Banza Stone' amezikwa jioni ya leo katika makaburi ya Sinza Jijini Dar es Salaam akisindikizwa na wanamuziki, wasanii wa filamu, wanasiasa na wadau mbalimbali wa staa huyo.

Mazishi ya aliyekuwa mwanamuziki wa muziki wa dansi nchini marehemu Banza Stone

Baadhi ya wanamuziki wakiwemo mwimbaji Ali Choki, Luiza Mbutu, Nyoshi el Sadaat, Jose Mara, Steve Nyerere, Patcho Mwamba, Mh John Mnyika na wengineo wengi wameongea na eNewz kuhusiana na jinsi wanavyomkubuka nyota huyo ambaye ameacha pengo kubwa katika sekta ya burudani nchini.

Marehemu Banza Stone ambaye ameacha mtoto wake wa kiume anayeitwa Hadji, alifariki siku ya Ijumaa nyumbani kwake Sinza Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mungu ailaze Roho ya marehemu Banza Stone mahala pema peponi. Amin