Saturday , 25th Jul , 2015

Michuano ya Kombe la Kagame inatarajiwa kumalizika kesho katika hatua ya makundi kwa kuwakutanisha mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga dhidi ya Khartoum ukitanguliwa na mchezo kati ya Gor Mahia na Telecom.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo, katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF, Mwesigwa Celestine amesema, timu zilizotolewa katika michuano hiyo zimeshaanza kuondoka ambapo baadhi ya timu zilipata changamoto mbalimbali kuhusu usafiri ambapo zilitatuliwa.

Mwesigwa amesema, hapo kesho Yanga itashuka dimbani kumalizia hatua yake ya makundi michuano hiyo ikipambana na Khartoum huku ukitanguliwa na mchezo kati ya Gor Mahia na Telecom ambayo imeshayaaga mashindano hayo.

Mwesigwa amesema, watanzania wanatakiwa kujitokeza kuzipa sapoti timu zilizobakia katika michuano hiyo ambazo ni Yanga na Azam FC huku KMKM ikiwa imeshatupwa nje ya michuano hiyo.