
Awali Yanga ilipeleka majina 24 CAF hivyo kuongezeka kwa majina hayo manne imeongeza idadi na kuwa na jumla ya wachezaji ni majina 28 na zinaendelea kubaki nafasi mbili.
Majina ya wachezaji wapya wa Yanga ambayo tayari yameshatumwa CAF ni Hassan Kessy aliyejiunga akitokea Simba SC baada ya mkataba wake na Simba kuisha, Juma Mahadhi akitokea Coastal union ya jijini Tanga, Andrew Vicent 'Dante' kutoka Mtibwa Sugar na Beno Kakolanya ambaye amejiunga nao akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya.