
kikosi cha Yanga kwenye picha ya pamoja kabla ya moja ya mechi za ligi kuu tanzania bara msimu uliopita
Akizungumza na East Africa Radio mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa wanajangwani hao Jerry Muro amesema kikosi chote kimewasili salama na hakuna majeruhi hivyo wanaimani wataibuka na ushindi kesho dhidi ya maafande wa Mgambo JKT.
Muro ametamba kuwa tayari wanayosiri ya ushindi wakiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ambao mara kadhaa umekuwa si rafiki kwa klabu kongwe ingawa msimu uliopita yanga ilipata matokeo mazuri huku simba ikifanya hivyo msimu huu.
Mara baada ya mechi ya kesho Yanga itasalia mjini Tanga kwa ajili ya mechi nyingine dhidi ya wanakimanumanu wa African Sports itakayopigwa kati kati mwa juma lijalo..