Wednesday , 6th Aug , 2014

Katibu mkuu wa Yanga amesema wamepokea barua kutoka TFF ikiwataarifu kuondolewa kwao kwenye mashindano kwa madai ya kukiuka kanuni. Lakini kanuni zenyewe hazikutajwa bayana.

Jengo la makao makuu ya Yanga:Twiga/Jangwani.

Klabu ya Yanga ya jijini DSM imeelezea kusikitishwa na kitendo cha waandaaji wa mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA kuiondoa timu hiyo kwenye mashindano ya mwaka huu kutokana na uvunjaji wa kanuni za mashindano hayo.

Akiongea leo jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Benno Njovu amesema wameonewa kwa sababu kanuni za wanazotuhumiwa kuzivunja hazikuwekwa wazi lakini wao kama Yanga wanahisi kwamba kanuni zinazozungumziwa na kikosi kilichopelekwa.

Bwana Benno Njovu amesema kimsingi wao walipeleka kikosi ambacho wao kama klabu waliridhika nacho na akaongeza kwamba imefikia wakati viongozi wa klabu na vyama vya mpira wakawaachia walimu kuchagua wachezaji na sio wao.

Naye kocha wa klabu hiyo, Mbrazil marcio Maximo amesema kikosi alichokichagua kwenda Kigali ni kile ambacho amekuwa akifanya nacho mazoezi kwa muda mrefu na kile alichokiacha ni kile ambcho kina wachezaji wengi waliokuwa timu ya taifa na waliosajiliwa hivi karibuni hivyo hawakuwa tayari kimazoezi kuingia kwenye mashindano makubwa kama hayo