Wednesday , 12th Aug , 2015

Mabingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Yanga wanatarajia kushuka dimbani leo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Maafande Tanzania Prisons.

Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc itakayochezwa Septemba 22 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam pamoja na Ligi Kuu Bara.

Yanga imeweka kambi mjini Tukuyu kujiandaa na michuano hiyo, na tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Kimondo ya Mbozi na kushinda kwa mabao 4-1.

Baada ya mechi hiyo, Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani siku ya jumapili kucheza dhidi ya Mbeya City.