Sunday , 14th Feb , 2016

Danny Welbeck ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu April mwaka uliopita ameifungia Arsenal bao la pili na la ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester.

Danny Welbeck ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu April mwaka uliopita ameifungia Arsenal bao la pili na la ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester.

Welbeck alimhakikishia Wenger ushindi huo muhimu uliotamatisha msururu wa mechi 16 bila kushindwa wa kocha Claudio Ranieri wa Leicister City.

Mchezaji mwingine wa akiba Theo Walcot ndiye aliyeisawazishia Arsenal kunako dakika ya 70 ya kipindi cha pili.

Wageni hao ambao wameshangaza wengi msimu huu walikuwa wamefunga bao la kwanza kupitia kwa mkwaju wa penalt likifungwa na Jamie Vardy kunako dakika ya 45'', baada ya kukwatuliwa ndani ya eneo la hatari na mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal.

Hadi mwisho wa mchezo, wenyeji Arsenal wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1.