Wednesday , 11th Jun , 2014

Baraza la wazee wa klabu ya Yanga wamelaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuendesha kampeni za chini chini kupinga kitendo cha nkutano mkuu wa June Mosi kuuongezea muda wa mwaka mmoja uongozi wa sasa wa klabu hiyo.

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga-Ibrahimu Akilimali

Baraza la wazee la klabu ya Yanga ya jijini DSM, umeelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha baadhi ya wanachama waonapinga maamuzi halali ya mkutano mkuu ya kuwaongezea muda viongozi wa sasa wa klabu hiyo.

Akiongea kwa niaba ya wazee wenzake, katibu wa baraza hilo mzee Ibrahim Akilimali amesema kimsingi mkutano mkuu wa June Mosi mwaka huu ulifanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya klabu hiyo hivyo wale wote wanaoyapinga maamuzi hayo hawaitakii mema klabu hiyo.