Wanariadha wa Tanzania wakichuana katika moja ya mashindano yaliyofanyika hapa nchini.
Rais wa shirikisho la riadha nchini Tanzania RT Anthony Mtaka amewataja wanariadha hao wanne watakaoshiriki katika michuano hiyo ya Afrika kusini itakayoanza Juni 22 mwaka huu kuwa ni pamopja na Fabian Sulle atakayekimbia mbio za mita 5000 na 10000.
Wengine ni Bazili Baynit atakayekimbia mita 1500, Ismail Juma na Joseph Theophil ambao wote watakimbia mita 10000.
Mtaka ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha mchezo wa tenisi Tanzania TTA kwa sasa ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema mbali na wanariadha hao kuendelea na maandalizi ya kushiriki mashindano hayo ya Afrika Kusini bado shirikisho RT inaendelea kusaka mashindano zaidi ya kimataifa ya kufuzu yatakayofanyika barani Afrika kwaajili ya kuongeza idadi ya wanariadha watakaokwenda Brazil kuwakilisha nchi baada ya kufikia viwango vya kufuzu Olimpiki.
Mtaka amesema baadhi ya wanariadha walijaribu kutafuta viwango katika michuano ya kimataifa nje ya Afrika hawakufanikiwa hivyo sasa RT inageukia michuano itakayofanyika barani Afrika ili kuona wanriadha wa Tanzania wanafikia viwango hivyo stahiki vya kushiriki michuano ya Olimpiki.
Mtaka amesema wanariadha Sara Ramadhan na wengine kama kina Fabiola William na Natalia Elisante ambao walikwenda nchini Macdeonia wamerejea nchini lakini hawakufanikiwa kufikia viwango vya kufuzu Olimpiki hivyo sasa RT inafanya njia mbadalah kuhakikisha wanapata nafasi ya mwisho ya kufuzu.
Hatua ya kukosa nafasi hiyo ama kutofikia viwango vya kufuzu ilimkuta pia mwanaridha Bazili Baynit ambaye alishiriki michuano ya kimataifa iliyofanyika nchini Sudan Mei 19 mwaka huu.