Tuesday , 26th Apr , 2016

Hatimaye shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania limefanikiwa kupata mchezo wa kujipima nguvu kwa ajili ya kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars kufanya maandalizi ya mchezo mgumu wa kufuzu AFCON dhidi ya Mafarao wa Misri.

Kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya (Harambee Stars) Mei 29, 2016 jijini Nairobi.

Mchezo huo wa kirafiki utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujaindaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.

TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.

Kikosi cha Taifa Stars kianchonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi Mei, mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika uwanja wa Taifa jijini Dra es salaam Juni 04, 2016.

Stars inajianda na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017 nchini Gabon dhdi ya Misri utakaochezwa Juni 04, mwaka huu.