Jumapili , 6th Jul , 2025

Mkongwe wa muziki kutoka Benin Angélique Kidjo, ametajwa na kuchaguliwa kuwa Mwafrika wa kwanza kupewa nyota ya Hollywood Walk of Fame duniani.

Picha ya Angelique Kidjo

Jina lake lipo kwenye orodha ya majina 35 yaliyotangazwa kupewa nyota hiyo ya heshima siku ya Julai 10 Los Angeles Marekani, pamoja na mastaa wengine kama Miley Cyrus, Timothée Chalamet, Demi Moore,Shaquille O'Neal.

Angelique Kidjo tayari ni mshindi wa tuzo 5 za Grammy, atapokea heshima hiyo baada ya kufanya muziki kwa zaidi ya miongo minne na kutoa Album 16.

Star Hollywood Walk of Fame ni heshima wanayopewa watu wenye mchango katika tasnia ya burudani kama waigizaji,wanamuziki,producers, directors na wana michezo wakubwa hivyo wanaheshimishwa hadharani kwa mafanikio yao na ushawishi mkubwa.