Friday , 15th May , 2015

Wachezaji nchini wametakiwa kuwa na jitihada binafsi katika michezo ili kutumia vizuri nafasi mbalimbali walizozipata.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini, Gulam Rashid amesema wanamichezo mbalimbali hususani riadha ambao wamepata nafasi ya kwenda katika mazoezi ya maandalizi ya michuano ya Olimpiki hapo mwakani.

Gulam amesema vijana hao wapatao watatu ambao ni Fabian Joseph, Bazil Boay na Fabian Nelson watashiriki mafunzo hayo ambayo yatafanyika Eldoret nchini Kenya ambapo wamethibitishwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa IAAF kwa kufuatana na sheria walizonazo.

Gulam amesema, wanariadha hao ambao mpaka Jumatatu wanatakiwa wawe wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya mazoezi hayo pia wanatakiwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo ili kuweza kudumu katika kambi hiyo na kuweza kufanya vizuri katika mashindano.