
Yury Gazinsky ameungana na wachezaji Neymar Jr wa Brazil na Siphiwe Tshabalala wa Afrika Kusini ambao wote walifunga mabao ya ufunguzi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 na 2014.
Pia mchezaji Denis Cheryshev wa Urusi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea benchi na kufunga mabao mawili kwenye mechi hiyo ya ufunguzi huku mabao mengine yakiwa yamepachikwa na Aleksandr Golovin pamoja na Artem Dzyuba.
Kwa upande mwingine, wenyeji Urusi wamendeleza rekodi ya timu mwenyeji kutofungwa kwenye mechi ya ufunguzi tangu fainali hizo zianzishwe mwaka 1930 nchini Uruguay.