
Mwenyekiti wa Chama cha soka wanawake Tanzania TWFA Amina Karuma amesema, Chabruma ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji katika timu hiyo itakuwa mechi yake ya mwisho ambapo atacheza dakika 45 za mwanzo na mchezo utasimamishwa kwa ajili ya kutoa historia yake kwa ufupi katika soka la wanawake hapa nchini.
Amina amesema, katika kumuenzi Chabruma, wameamua kumjumuisha kwenye benchi la ufundi la kikosi timu ya taifa ya Twiga Stars.