
Saimon Msuva (wa kwanza kulia) akiwa katika kipindi cha 5Sports cha EATV na watangazaji wa kipindi hicho kutokea kushoto ni Tom Chilala, Tigana Lukinja, na Ladislaus
Msuva amefunguka kuhusu utaratibu huo kupitia kipindi cha 5SPORTS kinachoruka kila Jumatatu saa 3:30 usiku kupitia EATV, na kubainisha kuwa lengo ni kujitafutia baraka zaidi kutoka kwa Mungu na pia kutoa shukrani.
Amesema tangu ajiunge na Yanga amekwisha cheza misimu mitatu na mwaka huu ukiwa ni msimu wa nne, na yote imekuwa ni ya mafanikio kwake ikiwemo kupata tuzo ya mchezaji bora wa msimu pamoja na tuzo ya mfungaji bora, na zote amezipeleka kuzihifadhi kanisani kulingana na malezi aliyolelewa na wazazi wake.
"Mimi nimelelewa maisha ya kidini, familia yetu ni watu wa imani, kwahiyo nimekuwa ni muumini mzuri na mara nyingi viongozi wangu wa kidini hunishauri mambo mbalimbali katika maisha, hata tuzo nilizopata nimezipeleka kanisani, naamini Mungu ndiye kila kitu kwangu"
Saimon Msuva akiwa Kikaangoni ya EATV
Akizungumzia mafanikio ya kimaisha aliyoyapata, Msuva amesema kupitia soka analopiga Yanga, hadi sasa amefanikiwa kuwa na nyumba mbili, moja akiwazawadia wazazi wake, pamoja na kumiliki gari mbili anazotumia katika kwa binafsi.
Pia msuva hakusita kuweka wazi mshahara analipwa na klabu ya Yanga kwa sasa kuwa ni shilingi za Kitanzania milioni 3 kwa mwezi, ambazo zinamsaidia kusukuma maisha pamoja na kulea wazazi wake, na mtoto wake mmoja aliyezaa na mchezaji wa Twiga Stars, Fatuma.
Akizungumzia mtu anayemsimamia katika kazi yake, amesema baba yake mzazi anayeitwa Happygod Msuva ndiye kila kitu, na ndiye meneja wake ambaye humuwakilisha katika mikataba pamoja na ushauri.
Saimon Msuva, akishangilia moja ya mabao aliyofunga msimu huu.
Katika msimu huu wa ligi, Msuva ameshaifungia timu yake ya Yanga mabao 7 katika mzunguko wa kwanza, akiwa sawa na Amis Tambwe kutoka klabu hiyo hiyo ya Yanga, huku wakitanguliwa na Shiza Kichuya kutoka Simba