Thursday , 5th Nov , 2015

Msimamizi wa mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana katika kituo cha michezo cha vijana cha Jakaya Kikwete JMK Youth Park Bahati Mgunda amesema, wapo katika mikakati ya kuwa na kliniki kwa ajili ya walimu wa michezo mashuleni.

Mgunda amesema, wanaamini kila shule katika nchi hii kuna walimu wa michezo lakini bado hawajajua yupo kwa upande wa michezo gani hivyo kliniki hiyo itawasaidia walimu kuweza kuwa na elimu ya kutosha kwa ajili ya kuwapa wanafunzi mafunzo ambayo yatawawezesha kufanya vizuri katika ligi ya mpira wa kikapu ya vijana kati ya miaka inatarajia kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi Februari mwakani.

Mgunda amesema, mafunzo kwa ajili ya walimu yatakuwa yakifanyika kabla ya msimu wa ligi, katikati ya msimu na mwisho wa msimu ambapo yatajumuisha walimu 30 wa shule shiriki za mkoa wa Dar es salaam.

Mgunda amesema, kwa upande wa wachezaji kutakuwa na mafunzo katikati ya ligi ambapo wataletwa walimu kutoka ligi kuu ya kikapu Marekani NBA ambapo watakuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi 100 kwa kila msimu wa ligi ambapo itafahamika kama Basketball Klinic for Players.