Friday , 5th Jun , 2015

Chama cha Mpira wa meza nchini TTTA kimeandaa mashindano ya taifa ya kuwasaka wachezaji watakaounda timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya kimataifa mwaka huu.

Katika taarifa yake, Katibu mkuu wa TTTA Issa Mtalaso amesema, mashindano hayo yamepangwa kufanyika Juni 20 hadi 25 Ukumbi wa Shule ya Msingi Kisutu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha wachezaji kutoka mikoa yote ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar.

Mtalaso amesema, mpaka sasa hawajapata timu itakayoshiriki mashindano ya All African Games, hivyo wameamua kuandaa mashindano hayo mapema ili kuweza kuandaa wachezaji watakaounda timu ya Taifa.

Mchezo wa mpira wa meza ni miongoni mwa michezo itakayoshiriki michuano ya All African Games Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.