Saturday , 2nd Aug , 2014

Chama cha mpira wa magongo Tanzania THA kimesema kinawapa michezo ya kujipima uwezo timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ili ipate uzoefu zaidi dhidi ya wanawake wenzao katika michuano ijayo ya kimataifa

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ya mpira wa magongo.

Timu Nne kati ya Tano za mpira wa magongo za mkoa wa Dar es salaam zinazotarajiwa kushiriki michuano ya Phonex itakayoanza August 8 mwaka huu jijini Tanga hii leo zimecheza ligi ndogo maalumu katika uwanja wa Lugalo ikiwa ni maandalizi ya timu hizo kuelekea michuano hiyo mikubwa

Katibu msaidizi wa chama cha mpira wa magongo Tanzania THA Mnonda Magani amezitaja timu tano za jeshi [TPDF] wanaume, kombaini ya wanaume, makongo sekondari na timu ya taifa ya wanawake ndizo zitashiriki michuano hiyo
Aidha Magani amesema lengo kubwa zaidi la ligi hiyo ni kuzianda timu za makongo sekondari na timu ya taifa ya wanawake zinazojianda na michuano ya kimataifa

Kwa upande wake nahodha wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa magongo ya Tanzania Kidawa Suleiman amesema kucheza michezo mingi ya kujipima uwezo hasa na timu za wanaume kutawapa uwezo mkubwa wa kuweza kupata matokeo mazuri katika mashindano yanayohusisha wanawake wenzao.