Mechi hizo zitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam ambapo mbali na mechi kati ya wenyeji Tanzania na Namibia itakayochezwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kenya, watacheza na Nigeria uwanja wa Gymkhana na Uganda watacheza na Botswana uwanja wa Annadil Burhani.
Wachezaji wa timu ya Tanzania ni pamoja na nahodha Arshan Jesani, Godluck Andrew, Salum Jumbe, Juma Mohammed, Shafii Kolo, John Ngati na Hamis Said.
Wengine ni Martin Kavuli, Rashid Awadhi, Umang Somanyi, Razaro Festo, Harshened Anant, Suleiman Nassoro, and Raheel Krishna ambapo watakuwa chini ya makocha Khalil Rehemtulla na Hamis Abdallah.
Michuano hiyo ni sehemu ya kufuzu kucheza kombe la Dunia litakalofanyika mwakani, Dhaka, nchinbi Nigeria.