
Kikosi cha Simba SC, kikiwa uwanjani.
Simba walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya Dakadaha FC ya Somalia na APR ya Rwanda huku ikienda sare ya 1-1 dhidi ya Singida United ambayo inashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza.
Kabla ya mechi hiyo, Gor Mahia FC kutoka Kenya wataanza kibarua cha hatua hiyo ya robo fainali kwa kucheza na Vipers SC kutoka Uganda kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi zote mbili zitachezwa katika Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ambao utachezwa saa moja usiku, huku zimeibuka tetesi kuwa Klabu ya Simba ipo kwenye mchakato wa kuachana na beki Muivory Coast, Pascal Serge Wawa kutokana na kutoonyesha uwezo mzuri katika michuano ya Kombe la Kagame.