Uongozi wa klabu ya Simba umekataa ombi la klabu ya Etoile Du Sahel waliloiandikia FIFA la kusogeza mbele deni wanaloidai klabu hiyo kuhusu malipo ya mchezaji wao wa zamani Emanuel Okwi.
Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema,makubaliano ya mwanzo waliyopatana kuhusu deni la dola laki 3 sawa milioni 600 za Tanzania yamepita muda na Etoile waliomba deni hilo lisogezwe hadi mwezi machi mwaka huu,lakini FIFA wakasema Simba ndiyo wenye maamuzi yote.
Okwi aliuzwa Etoile Du Sahel ya nchini Tunisia januari 2013 lakini hakukaa sana kabla ya kurudi mwishoni mwaka huo kwa madai ya kuidai timu hiyo malimbikizo ya mshahara wa miezi mitatu na kubaki nchini Uganda hadi aliporudi Tanzania na kusajiliwa na Yanga januari 2014.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda,alirejea kwenye klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba,katikati ya msimu wa 2014,kabla ya juni 2015 na kuelekea klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.

