Tuesday , 28th Apr , 2015

Serikali na jamii imetakiwa kujitokeza kwa ajili ya kusaidia timu shiriki za ligi za mikoa ili kuziwezesha kufanya vizuri na kuweza kushiriki ligi za juu zaidi.

Akizungumza na East Africa Radio, mwenyekiti wa klabu ya Lucent ya mkoani Ruvuma, Yusuph Lyambe amesema, michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei tisa mwaka huu katika viwanja mbalimbali nchini itatakiwa kuwa na msaada wa serikali au jamii ili kuweza kuipa sapoti ya mambo mbalimbali hususani vifaa vya michezo.

Lyambe amesema, misaada hiyo itaweza kusaidia timu hizo kuweza kujihakikishia kufanya vizuri katika michuano mbalimbali na kujipatia vipaji vipya vitakavyoweza kuitangaza nchi katika soka.