Tuesday , 5th Jul , 2016

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametetea uamuzi wa mreno Jose Mourinho kumbwaga Ryan Giggs katika cheo cha kocha msaidizi badala yake kumuita Rui Farria kutwaa nafasi yake.

Sir Alex Ferguson enzi zake akiwa kocha ndani ya Manchester United.

Ferguson amesema huo ni uamuzi sahihi kwa kocha huyo kwa kuwa ili afanye vyema kwenye kazi yake ni lazima akawajumuisha watu anaowaamini muda wote hivyo si jambo la kushangaza kwa Mourinho kumuamini Farria ambaye amefanya naye kazi kwa muda mrefu.

Uamuzi wa Mourinho kutaka kumpa majukumu mengine Giggs kumemfanya gwiji huyo aliyedumu na Manchester United kwa miaka ishirini na tisa kutimka klabuni hapo na kusaka maisha ya soka sehemu nyingine.

kuondoka kwa Giggs hakujasitisha mipango ya Mourinho ambaye mchana huu atazungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwake kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.