Wednesday , 1st Apr , 2015

Chama cha Riadha Nchini RT kimesema, Progamu ya watoto iliyoanza ambayo itadumu kwa muda wa wiki moja itasaidia vijana hao kuweza kujihusisha na michezo mbalimbali pamoja na kujiepusha na matendo maovu ambayo hayafai kwa jamii.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui amesema, anaamini watoto hao kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam watakapomaliza mafunzo hayo watakuwa wamepata somo kubwa sana kwa upande wa michezo litakaloweza kuwasaidia hata watakapo rudi katika masomo ya darasani.

Nyambui amesema, watoto hao ambao wanashiriki mazoezi ya michezo mbalimbali kama riadha na mpira wa miguu wataweza pia kujiajiri kupitia kimichezo pale watakapokuwa wamemaliza shule.