Thursday , 25th Jun , 2015

Mshambuliaji wa kimataifa wa Klabu ya Yanga, Mrundi Amisi Tambwe amesema, kuongezwa kwa idadi ya wachezaji wa kimataifa katika vilabu shiriki vya ligi kuu Soka Tanzania Bara itasaidia kuweka changamoto ya kiushindani.

Akizungumza na East Africa Radio, Tambwe amesema wanapokuwa wengi lazima wachezaji wazawa wajitume zaidi na haiwezi kushusha viwango zaidi ya kuchangia kuwapa nguvu kwani wanapokuwa wengi itamlazimu kila mchezaji kuweza kufanya vizuri.

Kwa upande mwingine Tambwe amesema, amejiwekea malengo ya kuwa juu zaidi ya wengine kwa kila timu anayochezea pamoja na kuiheshimu kazi yake ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya soka Afrika mashariki na kati maarufu kama Kombe la kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai mwaka huu.