Wednesday , 2nd Dec , 2015

Chama cha soka wilayani Mufindi kimewataka wadau wa wilaya hiyo kusaidia timu zilizopo ligi Daraja la kwanza ikiwemo timu ya Kurugenzi ili kuweza kupanga zaidi na kuweza kuongeza idadi ya timu shiriki za ligi kuu kwa Nyanda za Juu Kusini.

Katibu Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Festo Kilupamwambu amesema, wana nafasi kubwa kwa kutumia fursa katika mzunguko kuweza kupanda daraja kwani katika mzunguko wa kwanza timu hiyo ya Kurugenzi inashika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 14 huku anayeongoza akiwa na pointi 16.

Kilupamwambu amesema, wanahitaji kuwa na idadi kubwa ya timu za ligi kuu kwani mpaka sasa ukanda wa kusini ndiyo unaotoa vipaji vingi hivyo wanahitaji kuhakikisha wanakuwa na timu zaidi ya tano shiriki za ligi kuu tofauti na hivi sasa ambapo zipo timu tatu ambazo ni Tanzania Prisons, Mbeya City na Majimaji.