Tuesday , 26th Jan , 2016

Klabu ya Newcastle United imekubali kulipa dau la pauni milioni 12 kwa ajili ya kumsajili nyota wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Totenham Hotspurs Andros Towsend.

Nyota wa Totenham Hotspurs Andros Towsend anayewaniwa na Newcastle united.

Towsend mwenye umri wa miaka 24 anawaniwa na Newcastle united ambayo imekuwa na mwenendo mbaya msimu huu ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa EPL ikivuna alama 21 katika mechi 23 walizocheza.

Nyota huyo aliyejiunga na Spurs akiwa na umri wa miaka nane na kudumu nayo pasipo kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye timu ya wakubwa amecheza mechi tatu pekee za EPL katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo msimu huu.

Kocha mkuu wa Newcastle United Steve McLaren ameshafanya usajiri wa wachezaji Jonjo Shelvey kutoka Swansea na Henri Saivet kutoka Bordoux ya Ufaransa katika kipindi hi cha usajili.