Wednesday , 25th Mar , 2015

Ligi ya Mabingwa wa Taifa ya Mpira wa kikapu NBL inatarajia kuanza kutimua vumbi Mei nane mpaka 16 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa Mashindano TBF Michael Mwita amesema mashindano haya yatashirikisha timu zote za wanaume na wanawake, ili kuongeza ushindani zaidi.

Mwita amesema, viongozi wanatakiwa kutuma majina ya vilabu vitakavyo shiriki kutoka kwenye mkoa ili kuweza kuviweka katika mipango wakati wakiendelea kumtafuta mdhamini wa ligi hiyo.

Mwita amesema, washindi wanne wa Mashindano haya, kwa upande wa wanaume na wanawake watapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania bara kwenye Ligi ya Muungano hapo baadaye.