
Mapunda amesema, hajaona tofauti kubwa sana kati ya Simba SC alipotokea na alipo hivi sasa lakini anaamini alipo sasa anajifunza vitu vingi zaidi kutoka katika klabu hiyo.
Mapunda amesema, Azam FC imejaa wachezaji kutoka nchi mbalimbali wenye vipaji tofauti hivyo atajifunza zaidi sawa na kama angeondoka kwenda nje kwani atakutana na wachezaji ambao pia wana vipaji tofauti kama ilivyo kwa Azam FC.