Tuesday , 13th May , 2014

Bondia Francis Miyeyusho chichi mawe amewashukuru mashabiki wake pamoja na kundi lake la “Lazima Ukae Gym” kwa kumuunga mkono katika pambano lake la juzi dhidi ya bondia Mohamed Matumla.

Bondia Francis Miyeyusho

Bondia Francis Miyeyusho chichi mawe amewashukuru mashabiki wake pamoja na kundi lake la “Lazima Ukae Gym” kwa kumuunga mkono katika pambano lake la juzi dhidi ya bondia Mohamed Matumla

Miyeyusho amesema pamoja na kushinda mpambano huo kwa point lakini hakuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka kutokana na kutofanya maandalizi ya kutosha na hakuwa sawa kisaikolojia tangu apoteze mpambano wake wa kimataifa dhidi ya bondia toka nchini Thailand

Kauli hiyo iliungwa mkono na mama yake mzazi Bi Joyce Msumba ambaye naye alikiri mwanaye huyo kutokuwa katika kiwango cha kuridhisha katika mpambano huo japo anashukuru kwa kuwa alipata ushindi