Friday , 24th Jun , 2016

Klabu ya Mbeya City imemsaini kiungo mshambuliaji wa Tanzania Prisons Mohamed Mkopi kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mkopi ambaye alifanya vizuri kwenye msimu uliopita na kuisaidia klabu yake kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa VPL baada ya kufanikiwa kuvuna jumla ya pointi 51 katika michezo yake 30.

Nyota huyo aliweka wavuni magoli 6 katika msimu mzima, alichangia kwa kiasi kikubwa kung’ara kwa mshambuliaji Jeremia Juma wa Prisons kwa kumpikia magoli lukuki na kumfanya straika huyo kumaliza ligi akiwa na magoli 11.