Sane aliumia kwenye mchezo wa kombe la FA juzi dhidi ya Cardif City ambapo leo kocha wa kikosi hicho Pep Guardiola amesema nyota huyo atakuwa nje kwa takribani wiki saba.
Majeraha hayo yatamfanya Sane akose mechi ya fainali ya kombe la ligi EFL dhidi ya Arsenal mchezo utakaopigwa mwishoni mwa mwezi Februari.

Kwa mujibu wa ratiba ya EPL Sane pia atakosa mechi dhidi ya timu za West Brom, Burnley, Leicester, Arsenal na Chelsea pamoja na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wigan.
Mjerumani huyo mwenye miaka 22 amefunga mabao 11 na kusaidia kupatikana mengine 14 katika mashindano yote msimu huu hivyo Pep ameeleza kuwa ni pengo kubwa ukizingatia mshambuliaji mwingine Gabriel Jesus bado hajapona majeraha yake.

