Wamiliki hao pia wameomba msamaha kwa mashabiki wao kwa usumbufu walioupata tangu kutolewa kwa taarifa ya gharama mpya za tiketi kuwa paund 77 sawa na shilingi laki 2 na elfu 40 kutoka Paund 59 kwa mechi moja.
Maelfu ya mashabiki waliondoka katika uwanja wa Anfield kunako dakika ya 77 katika mechi dhidi ya Sunderland ili kupinga gharama hiyo.
Katika kurudisha bei ya awali wamiliki wa kilabu hiyo Fenway Sport waliwaambia mashabiki kwamba 'wamepata ujumbe'. Na kwamba sasa tiketi hizo sasa zitauzwa pauni 59.








