Tuesday , 24th Mar , 2015

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea hapo kesho kwa kuchezwa mechi kati ya Yanga wakiwakaribisha JKT Ruvu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mechi hiyo ni ya kiporo ambapo iliahirishwa ili kuipa Yanga nafasi ya kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Yanga inatupa karata yake ikiwa inaongoza katika msimamo wa Ligi kuu kwa kuwa na Pointi 37 ikiiacha Azam kwa Pointi moja huku JKT Ruvu ikiwa na Pointi 25.