Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakatamiwa wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
Katika Ligi hiyo, Yanga inaonekana kuchanja mbuga kuelekea ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, ambapo inaonesha wazi kuwa vita ipo kati ya Simba na mabingwa watetezi, Azam FC ya kugombania nafasi ya pili.
Azam imekumbwa na droo tatu mfululizo na kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 39, ikifuatiwa na Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 35.