Thursday , 5th Nov , 2015

Kocha mkuu wa Toto Africans Martin Grelic ameahidi kurejea katika timu hiyo endapo mambo aliyoomba kwenye barua yake kwa uongozi yatafanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Toto Africans Godwin Aiko amesema, Grelic tayari amerejea nchini Ujerumani kwa ajili ya mapumziko na amewaahidi kurea endapo watamtekelezea mambo aliyoomba.

Aiko amesema, katika barua Grelic ameomba timu kupatiwa mahitaji muhimu kama malazi, chakula pamoja na wachezaji kulipwa mishahara yao kwa wakati ili kuwawezesha wachezaji kujituma na hatimaye kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Kwa upande wake Afisa habari wa Toto Cathbeth Japht amesema, timu hiyo haina mpango wa kuajiri kocha mwingine baada ya Grelic kuondoka.

Japhet amesema, timu imefikia uamuzi huo kutokana na makocha wasaidizi wawili waliokuwa wakisaidiana na Grelic wana uwezo wa kufundisha.