
Msaidizi huyo wa zamani wa kocha aliyetimuliwa Claudio Ranieri, alitangazwa kuwa kocha Leicstere City hadi mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa Uingereza kushinda mechi mbili dhidi ya Liverpool na Hull katika EPL na kufufua matumaini ya kutoshuka daraja.
Leo kocha huyo, atawaongoza Mbweha hao, kwa mara ya kwanza kama kocha Mkuu, ili kupindua matokeo ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Sevilla, wiki mbili zilizopita.
Mchezo mwingine wa pili hii leo, ni pale mabingwa wa Italia Juventus, walioshinda mechi ya Kwanza 2-0 Ugenini, wapo kwao Juventus Stadium Jijini Turin, Italia kurudiana na FC Porto.
Kesho pia zitapigwa mechi 2 ambapo Atletico Madrid wako kwao Vicente Calderon Jijini Madrid, Hispania kulinda ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Wajerumani Bayer 04 Leverkusen, ilhali huko Ufaransa ambako AS Monaco wanapaswa kupindua kipigo cha 5-3 walichopewa na Manchester City.
Tayari timu 4 zimeshatinga robo fainali ya michuano hiyo kufuatia kukamilika kwa Mechi zao za pili za raundi ya mtoano ya timu 16 wiki iliyopita na wiki hii, Jumanne na Jumatano, zitapatikana Timu nyingine kutimiza idadi ya Timu 8.
Wiki iliyopita timu 4 za kwanza kutinga robo fainali ni Mabingwa watetezi Real Madrid, FC Barcelona, Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Ijumaa hii timu hizo 8 zitaingizwa kapuni kupanga Mechi 4 za robo fainali ambazo zitachezwa kuanzia Aprili 11.