
Emmanuel Mvuyekure mwenye jezi namba 10 mgongoni.
Afisa habari wa KMC, Anwar Binde ameithibitishia www.eatv.tv kuwa mshambuliaji wao huyo raia wa Burundi hatakuwa sehemu ya mchezo wa leo kutokana na kuumia mazoezini.
''Ni kweli Mvuyekure anakosekana leo, sababu ni kwamba aliumia kwenye maandalizi ya mchezo huo''. amesema Binde.
Mvuyekure mpaka sasa ana magoli 8 na ndiye kinara wa mabao ndani ya kikosi hicho kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara.
Idadi ya mabao ya Mvuyekure ni nusu ya yale ya mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere, ambaye mpaka sasa ana mabao 16.
#MICHEZO Kuelekea mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara leo kati ya KMC dhidi ya Simba, wachezaji wanao ongoza kwa magoli katika timu hizo ni Meddie Kagere (16) na Emanuel Mvuyekure (8). Mchezo utapigwa saa 10:00 jioni uwanja wa CCM Kirumba. pic.twitter.com/ueWYOr7rHp
— East Africa TV (@eastafricatv) April 25, 2019
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Simba ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 63 kwenye mechi 25, wakati KMC ikiwa katika nafasi ya 7 na pointi 42 katika mechi 32.