Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kila la heri Taifa Stars leo

Saturday , 15th Jul , 2017

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema kikosi chake kitaivaa Rwanda (Amavubi) bila kujali rekodi ya matokeo waliyopata katika mechi zilizopita hivi karibuni kwenye michuano ya Kombe la COSAFA.

Kikosi cha Taifa Stars

Akizungumza jana, Mayanga alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha leo wanaanza vyema safari ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Mayanga aliendelea kusema kuwa kikubwa katika mazoezi alikuwa anawajenga wachezaji kiakili na kujipanga kutowadharau wapinzani wao ambao nao wanataka kupata matokeo mazuri ugenini.

"Tunashukuru tumemaliza mazoezi ya mwisho asubuhi hii (jana asubuhi) kazi kubwa ya benchi la ufundi lilikuwa pia kuondoa uchovu walioupata katika mechi zilizopita na pia tumewaandaa wachezaji kuikabili Rwanda bila ya kuwa na kumbukumbu ya historia ya mechi zilizopita, tunajua Rwanda ina wachezaji wenye kasi na wenye morali ya kijeshi," alisema Mayanga.

Kwa mujibu wa Mayanga kikosi chake hakina majeruhi hata mmoja, huku nahodha Himid Mao, akisema kila mchezaji amejiandaa kupambana kwa ajili ya kusaka ushindi katika mechi ya leo.

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP