Timu ya watoto ya kikapu ikijiandaa kwenda nchini Canada
Wachezaji mchanganyiko wa mpira wa kikapu wa Tanzania waliokwenda nchini Canada kwa ajili ya mafunzo maalumu ya mpira wa kikapu kwa vijana wamerejea nchini hivi karibuni na kuanza kufanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo.
Kocha mkuu wa vijana hao ambao wengi wao wana umri chini ya miaka 12, Crey Bonner amesema vijana hao wamepata mafunzo ya kutosha na itakuwa ni faida kwa taifa kwa siku za usoni na amewaomba wadau na wadhamini kuendelea kudhamini safari za mafunzo kwa vijana wa michezo mbalimbali.
Crey amesema vijana wake hawakupata shida kwani walijiamini na ndio maaana walifanya vema katika mafunzo hayo.