
Juma Kaseja
Akiongea leo kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya timu yake ya KMC dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa leo kwenye uwanja wa mabatini Mlandizi Pwani, Kaseja amesema ameonesha timu hiyo ina mashabiki wa kweli hivyo anajihisi yeye na wenzake wanadeni la kulipa.
''Kwenye mechi ya kwanza tuliyotoa suluhu na JKT Tanzania kitu nilichoona ni wingi wa mashabiki wa timu yetu na jinsi walivyokuwa wakitushangilia hivyo nahisi leo pia itakuwa hivyo na lazima tuwalipe kwa kushinda'', amesema.
Kaseja kwa sasa ndiye nahodha wa KMC ambayo imepanda kucheza ligi kuu msimu huu na mchezo wa leo utakuwa ni wa pili kwao kwenye ligi kuu.