Beki wa Azam FC, Shomary Kapombe
Afisa habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, Shomary ambaye alikuwa na tatizo la Pulmonary Embolism ambalo ni damu kuganda kwenye mapafu alilopata msimu uliopita liliyomfanya kushindwa kuendelea na ligi huku Wawa naye wakiamua kufupisha likizo yake ili akaangaliwe afya yake mara baada ya kupata majeraha ya goti lake la kushoto kwa muda mrefu.
Maganga amesema, Azam wanahitaji wachezaji hao warejee uwanjani haraka kwani wamekuwa katika kipindi kigumu katika michezo mbalimbali kwa kuwakosa wachezaji hao ambao wanaumuhimu katika timu.
Kapombe alipata tatizo hilo la kiafya wakati Azam FC ikiwa mkoani Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Toto Africans ambapo Wawa alipata majeraha ya goti dakika za mwisho katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia.


