
Sam Allardyce
FA, ilikubaliana na Allardyce, kuvunja mkataba huo, kufuatia kocha huyo kuhusika na kashfa ya kuvunja kanuni za usajili za chama cha soka, baada ya kurekodiwa na chombo cha habari cha Telegraph akila njama hizo na waandishi waliojifanya mawakala wa kutoka Mashariki ya mbali, na kocha huyo, kuahidiwa angepewa pauni laki 4.
Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn amesema uamuzi wa kumfuta kazi Allardyce jioni ya jana ulikuwa mgumu lakini imefanyika hivyo kulinda heshima ya FA, baada ya wao kuona mkanda wa video wa tukio hilo.